Tanzania emblem

Gaming Board Of Tanzania

Ushering a New Era in the Regulation of Gaming Industry in Tanzania
GBT Logo

GBT YASAJILI KAMPUNI 91 ZA MICHEZO YA KUBAHATISHA

11 May, 2024
GBT YASAJILI KAMPUNI 91 ZA MICHEZO YA KUBAHATISHA

GBT YASAJILI KAMPUNI 91 ZA MICHEZO YA KUBAHATISHA.

Mkurugenzi Mkuu wa BODI ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, (GBT), James Mbaga, amesema kuwa hadi kufikia Juni 2023, Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania (GBT), imesajili jumla ya kampuni 91 zinazoendesha biashara za aina mbalimbali ya michezo ya kubahatisha nchini.

Mbaga amebainisha hayo alipokuwa akiwasilisha mada kuhusu mafanikio na utendaji wa Taasisi hiyo, katika kikao kazi kati ya Bodi hiyo, Wahariri wa vyombo vya habari, kilichofanyika leo Machi 6,2024 Jijini Dar es Salaam.

Amesema kuwa mwendeshaji sharti awe na leseni hai iliyotolewa na Bodi hiyo,  na kwamba michezo hiyo hairuhusiwi kuendeshwa katika maeneo yaliyopo Karibu na nyumba za ibada, shule, usalama, yasiyofikika kirahisi na maeneo ya kuendeshea biashara ya michezo ya kubahatisha, na kwamba kwa maeneo yaliyoruhusiwa sharti yawe yamesajiliwa na Bodi hiyo.

“Watoto wenye umri chini ya miaka 18 hawarusiwi kushiriki michezo ya kubahatisha kwani kwa kufanya hivyo ni kosa kisheria.

“Mwendeshaji sharti awe na leseni hai iliyotolewa na Bodi,  hivyo michezo hii hairuhusiwi kuendeshwa katika maeneo ambayo yamekatazwa kisheria” amesisitiza Mbaga.

Ameongeza kuwa, katika Jiji la Dar es Salaam zipo kasino nane, wakati Arusha na Mwanza kila mkoa zikiwa na kasino moja.

“Dar es Salaam inaongoza kwa kuwa na kasino nane, wakati Mwanza na Arusha kila mkoa una casino moja, sawa na asilimia 90 ya kasino zipo Dar es Salaam,” amesema Mbaga.

Amefafanua kuwa, kuna aina mbalimbali ya michezo ya kubahatisha ambayo ni michezo ya kibiashara kama kasino inayochezwa kwenye majumba maalum na mtandaoni, slot inayochezwa zaidi kwenye maduka maalum na baa, ubashiri wa matokeo ya michezo mtandaoni na madukani na bahati nasibu ya jumbe fupi za simu (sms lotteries).

Ameongeza kuwa, mchango wa sekta katika mapato ya serikali kodi imeongezeka kutoka shilingi bilioni 33.6 mwaka 2016/17 hadi kufikia shilingi bilioni 170.4 kwa mwaka 2022/23, ambapo ni sawa na ongezeko la wastani wa asilini 407.1 kwa mwaka katika kipindi hicho.

“Sekta ya michezo ya kubahatisha Tanzania tumefanikiwa kuzalisha ajira zilizo rasmi na zisizo rasmi zaidi ya 25,000. Hivyo sekta hii imefanikiwa kutoa mchango mkubwa katika uzalishaji wa ajira nchini,” amesema Mkurugenzi mkuu huyo.

NEWS LINK: GBT YASAJILI KAMPUNI 91 ZA MICHEZO YA KUBAHATISHA - habari mpya leo 2024 GREEN WAVES MEDIA